Wizara ya afya inasema imeweka mikakati murwa kuzuia Ebola

  • | Citizen TV
    362 views

    Kaunti 20 nchini ziko kwenye hatari ya maambukizi ya virusi vya Ebola vilivyoathiri watu 36 nchini Uganda kufikia sasa. Kwenye kikao kuhusu mikakati ya kuthibiti maambukizi ya virusi hivyo nchini, Mkurugenzi wa afya Dr.Patrick Amoth anasema wizara ya afya imeweka mikakati ya kutosha kuhakikisha Kenya inasalia salama na virusi hivyo hatari. Miongoni mwa mikakati ni kuwapima wanaoingia nchini kupitia kaunti za mpakani.