Wizara ya afya kuwapa chanjo watoto 131,000 dhidi ya malaria kwa kaunti zinazozingira ziwa Victoria

  • | Citizen TV
    263 views

    Wizara ya afya inalenga kuwapa chanjo watoto 131,000 dhidi ya malaria kila mwaka kwenye kaunti ndogo 25 zilizopo kwenye kaunti nne zinazozingira ziwa Victoria. Mkurugenzi mkuu katika wizara ya afya daktari Patrick Amoth amesema kuwa chanjo hiyo inayosambazwa kwenye kaunti za Kisumu, Siaya, Homa Bay, Vihiga, Busia, Bungoma, Migori na Kakamega ipo salama na imezaa matunda tangu kuanzishwa kwa kuwa imepunguza vifo vya watoto vinavyosababishwa na malaria.