Wizara ya elimu yaweka mikakati ya kuimarisha masomo

  • | Citizen TV
    125 views

    Wizara ya elimu kwa ushirikiano na hazina ya ustawi wa maeneo bunge -CDF- zimeanzisha juhudi za kurejesha hadhi ya shule ya upili ya wavulana ya St. Paul's Amukura iliyoko katika eneo bunge la Teso Kusini kaunti ya Busia. Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka wa 1962 ni miongoni mwa shule za upili tajika katika kaunti ya Busia zilizotia fora miaka ya tisini, ila matokeo ya mitihani ya kitaifa sasa yamedidimia zaidi .