Wizara ya fedha yatoa maependekezo ya jinsi inavyopanga kujisitiri kifedha kwa miaka mitatu ijayo

  • | K24 Video
    25 views

    Iwapo mapendekezo ya hazina ya kitaifa yatapitishwa kuwa sheria basi wakenya watalazimika kujizatiti na kulipa ushuru zaidi wakati huu wanapokabiliwa na wakati mgumu kiuchumi. Kulingana na mapendekezo ya hazina ya kitaifa ya udhibiti wa deni la kitaifa kwa miaka mitatu ijayo,ushuru wa ongezeko la thamani la bidhaa, (V.A.T) utaongezwa hadi asilimia 18 ,huku shule zinazotoa huduma zisizofungamana na masomo moja kwa moja kama vile kuogelea zikilazimika kulipa ushuru huo wa V.A.T.