Wizara ya michezo imekabidhi uwanja wa Kasarani kwa kamati andalizi ya CHAN

  • | Citizen TV
    1,003 views

    Serikali kupitia kwa wizara ya michezo imekabidhi rasmi uwanja wa kasarani kwa kamati andalizi ya chan humu nchini baada ya kukamilika kwa ukarabati tayari kwa michuano hiyo itakayoanza agosti pili. Akiongoza hafla hiyo, waziri wa michezo nchini salim mvurya amesema wizara yake imefanya kila kilichohitajika na shirikisho la soka barani afrika caf ili kufikia viwango vya kuandaa mchuano wa chan. Uwanja huo wa kasarani ndio utandaa fainali ya mchuano huo Agosti 30, pamoja na mechi nyengine za makundi.