YALIYOJRI KATIKA SIASA ZA MAREKANI WIKI HII

  • | VOA Swahili
    Marekani inakaribia takwimu za vifo laki tano vinavyotokana na Covid 19, ugonjwa ambao unasababishwa na virusi vya corona. Chanjo na kushuka kwa viwango vya maambukizi kumeongeza matumaini kwamba huenda maisha haraka yakarejea katika hali ya kawaida. Suala moja kuu, hata hivyo, ni kufunguliwa tena kwa shule. Michelle Quinn anaripoti na Harrison Kamau anaisoma ripoti kamili. #DC #VOA