Zaidi ya wafanyakazi wa ndani 100 wahamiaji watelekezwa nje ya ubalozi Beirut Lebanon

  • | BBC Swahili
    Uchumi wa Lebanon unaporomoka na sarafu ya nchi hiyo ikikadiriwa kupoteza takriban 70% ya thamani yake katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Mamilioni ya watu waliokuwa na uwezo wa kujimudu kifedha sasa wamejipata hawawezi kugharamia chakula na mahitaji yao. Hali hii ya kiuchumi imesababisha zaidi ya wafanyakazi wahamiaji 100 raia wa Ethiopia kutelekezwa nje ya ubalozi wao siku za hivi karibuni kwa sababu waajiri wao wameshindwa kuwagharamia. #Beirut #Ethiopia #uchumi