Zaidi ya wakaazi 30,000 Mtito Andei kunufaika na mradi wa maji

  • | Citizen TV
    111 views

    Zaidi ya familia elfu 30 katika eneo la Mtito Andei kaunti ya Makueni wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kukamilika kwa mradi wa kuhifadhi maji katika mto Ngai Ndethya. Hii sasa ikikamilisha mahangaiko ya wakaazi ya muda mrefu kutembea safari ndefu kutafuta maji. Na kama Michael Mutinda anavyoarifu, mradi huo ulitekelezwa na mashirika yasio ya kiserikali ni mojawapo ya mikakati iliyowekwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi