- 219 viewsDuration: 2:32Zaidi ya wanafunzi 2000 kutoka familia maskini katika eneo bunge la webuye magharibi, kaunti ya bungoma Wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea sare rasmi za shule. Wadau wa elimu eneo hilo wamesema hatua hiyo ni mojawapo ya mbinu za kufanikisha elimu kufuatia mtafaruku wa sare ambapo baadhi ya walimu wakuu na madalali wameshtumiwa kwa kushiriki biashara hiyo na kupandisha bei ya sare maradufu. Wazazi wamepongeza mpango huo ambao ulilenga wanafunzi wa gredi ya kwanza hadi sita wakisema utasaidia kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila unyanyapaa wa kukosa sare zinazohitajika.