- 1,883 viewsDuration: 2:36Zaidi ya wapiga kura elfu sabini katika eneo bunge la isiolo Kusini, pamoja na wodi tatu za eneo la Kabras na Mbeere North wanatarajiwa kupiga kura hapo kesho kuwachagua viongozi wapya. Tume ya uchaguzi nchini IEBC ikisema matayarisho yamekamilika katika eneo bunge hilo pamoja na maeneo wodi ya Kabras West magharibi, Evuvore na Muminji huko Mbeere North. Kinyanganyiro cha ubunge cha Isiolo Kusini kinashindaniwa na mtu na nduguye wakitaka kumrithi baba yao Mohamed Tubi Bidu aliyefariki mwaka jana