Zaidi ya watu 25 walifariki nchini kwenye maandamano miongoni mwao akiwa msichana wa miaka 12

  • | Citizen TV
    9,430 views

    Idadi ya waliofariki katika maandamano ya siku ya saba saba kote nchini imefikia zaidi ya watu 25. Miongoni mwa waliofariki ni msichana wa miaka 12 aliyepigwa risasi akitazama televisheni na mamake ndani ya nyumba yao huko Ndumberi. Msichana huyo alikuwa kwao takriban kilomita mbili kutoka kwenye barabara ambapo maandamano yalikuwa yakiendelea.