Zaidi ya watu 4,000 wamewachwa bila makao nchini kutokana na mafuriko

  • | Citizen TV
    3,739 views

    Zaidi ya watu elfu nne wamewachwa bila makao kufuatia mvua kubwa inayonyesha sehemu mbalimbali nchini. Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu, zaidi ya watu elfu 20 wameathirika na mvua hii katika kaunti 16 nchini. Haya yakijiri huku athari za mvua zikiendelea kushuhudiwa mitaa mbalimbali ya Nairobi na hata kaunti za Tana River ambako mto Tana umeanza kufurika na kusababisha hofu ya kuvunja kingo zake.