Skip to main content
Skip to main content

Zaidi ya watu 700 waachwa bila makao kufuatia mafuriko eneo la Odiria, Busia

  • | Citizen TV
    127 views
    Duration: 1:44
    Zaidi ya watu 700 eneo la Odiria, Teso Kusini kaunti ya Busia wameathirika na mafuriko huku ekari 500 za shamba zikiharibiwa kabisa na maji ya mafuriko. Mvua kubwa eneo hili ikitatiza masomo katika shule ya msingi ya Odiria na kuwalazimu wanafunzi kusalia nyumbani. Wakaazi wamesisitiza kuwa ni sharti mabomba ya kuzuia maji yajengwe katika mto Malakisi ili suluhu ya kudumu ipatikane huku baadhi ya waathiriwa wa mafuriko wakikumbwa na magonjwa ya pumu na yale yanayosababishwa na maji taka. Mvua imekuwa ikinyesha eneo hili la Teso kusini ambako sasa wakazi wametakiwa kuhamia maeneo salama