- 3,595 viewsDuration: 7:26Katika siku ya 4 ya makabiliano yanayoshuhudiwa katika eneo la Mashariki ya Kati, Israel imetekeleza mashambulizi mapya dhidi ya Iran na vile vile katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Iran imeendelea kulengwa na mashambulizi - huku mji mkuu Tehran ukishuhudia mashambulizi kadhaa hii leo. Shirika moja la kutoa misaada ya kibinadamu, limesema kwamba zaidi ya watu 800 wameuawa nchini humo. #DiraYaDuniaTV