- 28,032 viewsDuration: 2:25Ziara ya Trump nchini China inaweza kuonekana kama siasa za mbali kati ya mataifa makubwa, lakini athari zake zinaweza kufika moja kwa moja kwenye maisha yako, kuanzia kwenye bei ya mafuta, gharama za bidhaa sokoni hadi nafasi za biashara na ajira katika Afrika Mashariki. Donald Trump yupo mjini Beijing kwa ziara ya kiserikali inayobeba ujumbe mkubwa kuhusu nguvu ya uchumi, biashara na ushawishi wa dunia. Huu si mkutano wa kawaida wa viongozi wawili; ni mazungumzo yanayoweza kuamua mwelekeo wa uchumi wa dunia katika kipindi ambacho mataifa mengi, ikiwemo ya Afrika Mashariki, yanategemea sana biashara kati ya Marekani na China Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw