Zoezi la kubomoa linaendelea kwa siku ya 4 hii leo Mavoko

  • | Citizen TV
    309 views

    Ubomoaji katika ardhi tata ya Mavoko kaunti ya Machakos inatarajiwa kuendelea kwa siku ya nne hii leo. Zaidi ya familia elfu kumi zimeathirika na ubomoaji wa majumba katika ardhi hiyo, huku wamiliki wa majumba wakiendelea kukadiria hasara baada ya nyumba zao kubomolewa. Baadhi ya waathiriwa wakisimulia safari zao kumiliki mali zilizoharibiwa huku shughuli katika eneo hili zikitatizwa kutwa nzima.