Zoezi la kutafuta miili katika mto Muswii linaendelea siku 4 baada ya ajali

  • | Citizen TV
    2,176 views

    Zoezi la kutafuta miili zaidi ya waliosombwa na maji katika mto kwa muswii huko makueni limeingia siku ya nne hii leo. Miili kumi tayari imepatikana kufikia sasa. watu hao walikufa maji baada ya lori walilokuwa wameabiri kujaribu kuvuka mto na kusombwa na mafuriko. Michael Mutinda amejumuika na Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Jrn ambaye anazuru eneo la mkasa.