Zoezi la mwigo la kukabiliana na moto lazua kiwewe katika jumba la KICC

  • | KBC Video
    43 views

    Wazima moto wa kaunti ya Nairobi kwa ushirikiano na kundi la ushirikishi wa usimamizi wa majanga waliandaa zoezi la mwigo kuhusu kukabiliana na moto katika jumba la mikutano la Jomo Kenyatta. Hatua hiyo iliibua taharuki miongoni mwa wageni na wafanyakazi wa jengo hilo ambao hawakuwa na uelewa wa matukio hayo. Iliwachukua maafisa hao dakika tano kumuondoa mtu wa kwanza aliyedaiwa kuwa mwathiriwa kutoka ndani ya jingo hilo. Zoezi hilo lilijiri saa chache kabla ya rais William Ruto kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa huduma zaidi za serikali mitandaoni. Ripota wetu Abdiaziz Hashim alishuhudia zoezi hilo na akakatuandalia taarifa ifuatayo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #darubini #firedrill