Madeni ya serikali | Serikali kuu na zile za kaunti zadaiwa shilingi billioni 696.9

  • | Citizen TV
    1,597 views

    Madeni ya serikali kuu na zile za kaunti yamefikia shilingi bilioni 696.9 kufikia mwisho wa mwezi machi mwaka huu. Kwa mujibu wa waziri wa hazina kuu ya kitaifa, kupanda kwa madeni haya kumeathiri pakubwa biashara ndogo nchini. Kutokana na haya, waziri anasema wametoa ombi kwa baraza la mawaziri kubuni kamati maalum kutathmini madeni yote na kubaini namna yatakavyolipwa.