Mlemavu aliyekatwa miguu yote mwenye ndoto ya kufika Mlima Everest

  • | BBC Swahili
    456 views
    Hari Budha Magar alikatwa miguu yake yote miwili kuanzia kwenye goto mnamo mwaka wa 2010 baada ya kukanyaga kwa bahati mbaya kifaa cha kulipuka alipokuwa akihudumu katika kikosi maalumu cha jeshi 'Gurkha' nchini Afghanistan. Brigedia ya Gurkhas ni jeshi maarufu la Nepali lililokuwa likipigana upande wa jeshi la Uingereza. Sasa, akiwa na umri wa miaka 43, analenga kuwa mtu wa kwanza aliyekatwa miguu juu ya goti kupanda Mlima Everest mwezi Mei. #bbcswahili #uingereza #everest