Ongezeko la wakimbizi Tanzania

  • | BBC Swahili
    1,048 views
    Nchini Tanzania kumeshuhudiwa ongezeko la wakimbizi zaidi ya 8,000 tokea mwezi Machi mwaka huu wakiomba hifadhi kutoka DRC. Wengi wa wakimbizi hao ambao ni wanawake na watoto wanatajwa kuondoka kutokana na vita vinavyoendelea Mashariki mwa DRC. Shirika la wakimbizi duniani UNHCR linasema jitihada za makusudi zinahitajika ili kurekebisha hali ya mambo Mashariki mwa DRC. Mwandishi wa BBC David Nkya ameandaa taarifa ifuatayo kutoka Kigoma Magharibi mwa Tanzania. #bbcswahili #tanzania #kigoma