Polisi waiomba mahakama kumzuilia mhubiri Ezekiel Odero kwa siku 30

  • | Citizen TV
    7,097 views

    Polisi wameiomba mahakama ya Shanzu kaunti ya Mombasa kumzuilia mhubiri Ezekiel Odero kwa siku thelathini ili waweze kukamilisha uchunguzi dhidi yake. Maafisa wa polisi wanachunguza hatia kadhaa za mhubiri huyo ikiwemo ulanguzi wa fedha, mauaji, kusaidia watu kujitoa uhai na kufundisha itikadi kali pamoja na kutesa watoto. Ezekiel alikamatwa jana baada ya kujiwasilisha polisi na kuhojiwa kwa saa kadhaa. aidha kwenye stakabadhi za polisi mahakamani, majasusi wanauhakika kuwa watu kadhaa wa kanisa lake la New Life Prayer Centre walifariki kati ya mwaka uliopita na mwaka huu.