Wafuasi wa Mbunge wa Maragua Mary Wamaua na mwakilisha wa wanawake Betty Maina wakabiliana Murang'a

  • | Citizen TV
    2,025 views

    Vita vya ubabe wa kisiasa vilisheheni eneobunge la Kigumo kaunti ya Murang’a, baada ya mwakilishi wa kike wa kaunti hiyo Betty Maina kuzomewa na umati. Maina alimshutumu mbunge wa eneo hilo Mary Waithira kwa kufadhili rabsha zilizoshuhudiwa huku akisema kuwa hatobanduka katika safari yake ya kisiasa. Hafla hiyo ya kuwasaidia kina mama wanaoshona vikapu iliyohudhuriwa na mawaziri watatu akiwemo waziri wa ardhi Alice Wahome ilisitishwa kwa muda, huku polisi wakirejesha hali ya utulivu