- 25,946 viewsDuration: 4:06Upasuaji wa miili ya watu waliouawa katika uwanja wa Kasarani na Nyayo wakati wa maombolezi ya marehemu waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, umethibitisha kuwa walifariki kwa kupigwa risasi. Risasi zilizopatikana kwenye miili ya Evans Kiche pamoja na Vincent Otieno Ogutu zimekabidhiwa mamlaka ya IPOA kwa uchunguzi zaidi. Hata hivyo, mwili mmoja umesalia makafani ya City bila kutambuliwa.