Skip to main content
Skip to main content

Mange Kimambi ashtakiwa

  • | BBC Swahili
    124,326 views
    Duration: 2:59
    Serikali ya Tanzania imemfungulia mashtaka ya kiuchumi mwanaharakati Mange Kimambi ambaye ana maskani yake nchini Marekani. Tovuti rasmi ya mahakama nchini Tanzania, inaonesha kuwa kesi hiyo itatajawa kwa mara ya kwanza alhamisi wiki hii- tarehe 4 disemba na inataja muda na hakimu aliyepangwa kuisikiliza kesi hiyo. Hakuna maelezo zaidi katika tovuti juu ya makosa yanayomkabili Mange, lakini hatua hii inakuja mwezi mmoja baada ya mwanasheria mkuu wa serikali nchini humo Hamza Johari kumlaumu mwanaharakati huyo kwa kuchochea maandamano ya ghasia yaliyotokea katika siku ya uchaguzi. Johari alisisitiza kuwa watachukua hatua dhidi ya mwanaharakati huyo na kusema kuwa lazima akamatwe. Lakini Je, Mange Kimambi ni nani hasa? Mwandishi wa BBC Laillah Mohamed @mrs.tadicha na uchambuzi wa kina. 🎥: @frankmavura 📷 Ikulu,IG Mangekimambi - - #bbcswahili #tanzania #siasa #maandamano #uchaguzimkuu2025 #mangekimambi