- 1,504 viewsDuration: 2:48Familia za watu kumi waliofariki kwenye ajali ya barabarani jumapili usiku katika eneo la Chabera, Homa Bay zimeandaa ibada ya pamoja ya wafu siku ya jumanne kabla ya mazishi. Familia hizo zimeanza maandalizi ya mazishi huku bi harusi, ambaye jamaa hao walifariki wakitoka kwenye harusi yake, akizungumzia mkasa huo uliogeuza siku ya furaha kuwa ya majonzi.