- 16,552 viewsDuration: 1:30'Sina ugomvi na mtu yeyote anayepigania amani. Lakini nikuambia kwamba, kwa hakika, huwezi kuwa na amani bila haki. Amani na haki ni vitu viwili vinavyotegemezana.'' - Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Tanzania, Juda Thaddeus Ruwa'ichi, amesema Watanzania wengi hawashabikii haki wala siyo wadau wa haki. Askofu Ruwa'ichi aliyasema hayo katika misa ya mkesha wa Krismasi jijini humo. "Ewe Mtanzania kama utaka kujigamba kuwa mtu wa amani, jitose kupigania haki, jitose kusema kweli, amani na mambo yanayompendeza Mungu," - Kumekuwa na mgawanyiko baina ya viongozi hususan wa dini wanaosisitiza sharti kuwe na amani na wale wenye wanaosisitiza kupigania haki ya watanzania kabla na baada ya vitendo vya uvunjifu wa amani, vurugu, machafuko na mauaji yaliyotokea siku na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 nchini Tanzania. - - - #krismas #wakristo #tanzaniatiktok #amani #bbcswahili Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw