- 18,055 viewsDuration: 3:21Kesi ya mauaji ya mwalimu na mwanablogu Albert Ojwang imeendelea mahakamani kwa siku ya tatu huku Ushahidi wa picha za CCTV ukionyesha jinsi marehemu Ojwang alivyosafirishwa kwa gari la polisi hadi hospitali ya Mbagathi katika njia ya kutatanisha. Shahidi na afisa wa mamlaka ya kusimamia utendakazi wa polisi IPOA Joshua Mutua akiieleza mahakama kuwa Picha hizo za CCTV zinaonyesha namna polisi walivyojikokota kabla ya kumwasilisha Ojwang kwa hospitali usiku huo.