- 316 viewsDuration: 2:11Serikali imetoa makataa ya siku tano kwa watu wanaodai kumiliki ardhi ya misitu katika maeneo ya Makunga, Ex-Smith, Rest, Teldet, misitu ya Triangle na shamba la Shirika la Ustawishaji Kilimo nchini ADC la Japata, Kaunti ya Trans Nzoia, kuondoka mara moja. Hatua hiyo inalenga kutoa nafasi kwa mazungumzo ya maridhiano na kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.