- 386 viewsDuration: 3:19Huku taifa likijiandaa kwa masomo ya gredi ya kumi, walimu katika shule za upili wamepewa fursa ya kujifunza kuhusu mtaala wa CBE kupitia tovuti ya KNEC. Akifanya tangazo hilo, afisa mkuu mtendaji wa baraza la mitihani nchini David Njegere alisema kuwa kozi hiyo inatolewa bila malipo kwa walimu waliosajiliwa na TSC kama mojawapo ya mikakati ya kuimarisha elimu chini ya mtaala wa CBC.