Skip to main content
Skip to main content

Mirengo kinzani yaibuka chamani ODM, viongozi chamani wasisitiza migogoro itatuliwe

  • | KBC Video
    13,488 views
    Duration: 5:28
    Chama cha ODM kinakodolewa macho na wimbi la mabadiliko katika uongozi wake iwapo tangazo la mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Winnie Odinga ni la kuaminiwa. Akizungumza kwenye uwanja wa Kamukunji katika eneobunge la Kibra, Winnie Odinga amesema atafanya kila juhudi kuhakikisha kuna mkutano wa kitaifa wa wajumbe wa chama hicho ili kubaini mwelekeo wa uongozi chamani kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Huku Abdiaziz Hashim akitupakulia taarifa kwa kina, Winnie amesisitiza azma yake ya kumuunga mkono katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna pamoja na mbunge wa Embakasi Babu Owino licha ya baadhi ya viongozi kutoa wito wa kutimuliwa kwao. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive