- 17,894 viewsDuration: 1:14Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa Ufaransa inapendelea “heshima badala ya vitisho” na akapinga vikali vitisho vya ushuru wa ziada. Akiwa katika Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) nchini Uswisi, Rais huyo wa Ufaransa alitoa kauli hiyo kufuatia tishio la Rais wa Marekani Donald Trump la kutoza ushuru kwa nchi zitakazopinga mipango yake ya kuiteka Greenland. “Hapa, katika kitovu cha bara hili, tunaamini kwamba tunahitaji ukuaji zaidi na utulivu zaidi duniani, lakini tunapendelea heshima badala ya uonevu,” @mariammjahid anaelezea kwa kina #bbcswahili #ufaransa #marekani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw