- 15,084 viewsDuration: 28:10Tunaanzia Kenya, ambapo wasafiri wamepata afueni baada ya wafanyakazi katika viwanja vya ndege kusitisha mgomo ambao ulitatiza safari za ndege katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu. Mgomo hupo ulianza jana Jumatatu na kuendelea hadi leo Jumanne, na umesababisha usumbufu mkubwa wa safari za ndege. Foleni ndefu zilishuhudiwa katika viwanja vya ndege, huku wasafiri wakisubiri kwa saa nyingi ndani ya vituo kujua hatima ya safari zao za ndege. Wafanyakazi hao walifanya mgomo kulalamikia kukwama kwa makubaliano ya ajira, miongoni mwa masuala mengine. Awali, chama cha marubani nchini Kenya kilionya kwamba mgomo huo unaweza kudhoofisha hali ya usalama wa usafiri wa anga, kwani ungevuruga ratiba ya wafanyakazi na kuongeza hatari ya uchovu. #Kenya #JKIA #bbcswahili #bbcswahilileo #tundulissu #Tanzania #Trump Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw