Skip to main content
Skip to main content

Serikali yatenga Ksh. 205M za kuwalipa waathiriwa wa wanyamapori E. Marakwet

  • | Citizen TV
    248 views
    Duration: 1:32
    Waziri wa Utalii na Wanyamapori Rebecca Miano, ametangaza kuwa wakazi 335 katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet, walioathiriwa na wanyamapori, watapata fidia zao ifikapo Juni mwaka huu. Hatua hii inawalenga hasa wale wanaoishi karibu na Mbuga ya Wanyamapori ya Rimoi. Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanyamapori Duniani iliyofanyika katika mbuga hiyo, Waziri Miano alidokeza kuwa serikali tayari imetenga shilingi milioni 205 kwa ajili ya kuweka ua kuzunguka mbuga hiyo. Mradi huo unalenga kuzuia mashambulizi ya mara kwa mara ya wanyama na kukomesha migogoro inayoshuhudiwa katika eneo hilo.