- 139 viewsDuration: 1:15Gavana wa kakamega Ferdinand Barasa ametangaza kwamba Hospitali ya mafunzo na rufaa ya kakamega itakuwa tayari kutumika ndani ya miezi mitano ijayo. Barasa alitoa taarifa hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa kazi za ujenzi zinazoendelea katika hospitali hiyo, ambapo alitathmini maendeleo yaliyopatikana hadi sasa. Alionyesha kuridhika na kasi ya mradi huo.