- 674 viewsDuration: 1:29Gavana wa Isiolo Abdi Guyo amefanya mabadiliko makubwa katika serikali ya Kaunti hiyo baada ya kunusurika kwenye jaribio la kufurushwa ofisini. Guyo aliwafuta kazi mawaziri wawili, akamwondolea majukumu Naibu Gavana na kupunguza idadi ya maafisa wakuu kutoka 31 hadi 21. Guyo alitangaza hayo kupitia taarifa rasmi ya amri ya utendaji iliyosomwa na mratibu wa mawasiliano wa Kaunti hiyo, Hussein Salesa.