Skip to main content
Skip to main content

Apanda jengo refu la Taiwan bila kutumia kamba

  • | BBC Swahili
    13,809 views
    Duration: 1:06
    Mpandaji wa Marekani, Alex Honnold, amefanikiwa kupanda jengo refu la Taiwan bila kutumia kamba, mkanda wa usalama au vifaa vyovyote vya kujikinga. Jengo hilo, linaloitwa Taipei 101 kwa sababu ya idadi ya sakafu zake, lina urefu wa mita 508 (futi 1,667) na limetengenezwa kwa chuma, vioo na saruji, likiwa limeundwa kufanana na shina la mianzi. Honnold anajulikana kwa kuwa mtu wa kwanza kupanda mwamba wa wima wa El Capitan, uliopo katika hifadhi ya taifa ya Yosemite huko California bila kutumia kamba au vifaa vya usalama. #bbcswahili #taiwan #mkweamajengo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw