- 147 viewsDuration: 2:02Zaidi ya miaka kumi baada ya uanzilishi wa mfumo mpya wa elimu nchini CBE, bado shule nyingi za umma zinakabiliwa na changamoto ya vifaa hitajika vya masomo ya Sayansi na hata maabara. Katika shule ya msingi ya Sinoko DEB kwenye Eneobunge la Kanduyi katika kaunti ya Bungoma, Mwalimu mkuu Anne Aketch anasema kuwa wanafunzi wake husoma tu ila masomo yanayohitaji Mazoezi ya vitendo yamesalia kuwa Ndoto.