Skip to main content
Skip to main content

Bekky Akolong avunja mila na kuwa fundi bomba

  • | Citizen TV
    1,051 views
    Duration: 3:05
    Katika makala yetu ya Mwanamke Bomba wiki hii, Bekky Akolong anasimulia jinsi alivyokabiliana na vikwazo vya mila na kuingia katika kazi ya ufundi bomba, inayotambulika zaidi kama taaluma ya wanaume. Akolong, ambaye pia ni mama, amesalia imara akisema kazi hii inamsaidia kukidhi mahitaji ya mwanawe na familia yake. Anasimulia namna alivyokabiliana na changamoto za kukosolewa na jamii kwa madai ya kukaidi tamaduni, akisisitiza kuwa ufundi bomba ni ndoto yake ya maisha.