- 3,344 viewsDuration: 3:01Maandalizi yameshika kasi kwa hafla rasmi za kumbukumbu ya marehemu waziri mkuu wa zamani Raila Odinga huko Bondo, kaunti ya Siaya. Wageni wameanza kuwasili kwa hafla hizo zitakazoanza katika uwanja wa Migwena hapo kesho, ambapo jamaa na marafiki wa Odinga watafika kumkumbuka mwaka mmoja baada ya kifo chake. Katika makazi ya familia ya Kang'o ka Jaramogi, mishumaa imewashwa usiku huu katika sehemu ya kumbukumbu hizi. Laura Otieno yuko huko na anaungana nasi kutoka Kang'o ka Jaramogi.