- 726 viewsDuration: 2:58Huku tahadhari ya mafuriko ya mvua ikitolewa kuanzia mwisho wa mwezi huu, maandalizi yanaendelea katika maeneo yaliyo katika hatari ya mvua za El Niño. Kinaya kikiwa bayana katika eneo la Budalangi, kaunti ya Busia, ambako baadhi ya waathiriwa wa mafuriko ya mara kwa mara bado wanaishi kwa hofu, huku sehemu nyingine zikishuhudia matumaini mapya. Wakulima katika maeneo hayo sasa wanajiandaa kwa msimu wa upanzi, licha ya hofu ya mafuriko yanayoweza kutokea. Laura Otieno ana taarifa zaidi.