Skip to main content
Skip to main content

DCI Pwani yaonya watu dhidi ya kusambaza uvumi kuhusu madai ya watu kupoteza sehemu zao za siri

  • | Citizen TV
    480 views
    Duration: 1:26
    Idara ya upepelezi eneo la Pwani imetoa onyo kwa watu wanaoeneza hofu kuhusu madai ya watu kupoteza sehemu zao za siri kaunti ya Mombasa. Kwa mujibu wa msimamizi wa kitengo hicho pwani Benson Kasyoki, taarifa hizi za porojo zimezua hofu miongoni mwa wakazi, akisema maafisa kutoka vitengo mbalimbali vya usalama wameanza kuwaandama wanaosambaza habari hizo za kupotosha. Imeripotiwa kuwa visa 19 vinavyohusishwa na ripoti hizi vimeandikishwa kaunti za Kwale, Kilifi na Mombasa na kusababisha kuteketezwa kwa washukiwa wawili