Skip to main content
Skip to main content

DCI yachunguza sakata ya ufujaji wa Shilingi bilioni 6.2 kwenye mishahara ya serikali

  • | Citizen TV
    811 views
    Duration: 2:50
    Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI, imeanzisha uchunguzi kuhusu kutoweka kwa shilingi bilioni 6.2 kutoka idara 12 za serikali kufuatia ukaguzi uliofanywa kuhusu sakata ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali. Akikabidhi ripoti hiyo kwa Mkurugenzi wa DCI, Mohamed Amin, Waziri wa Utumishi wa Umma, Geoffrey Ruku, amesema serikali imejizatiti kukomesha wizi wa fedha za umma na kuhakikisha waliohusika wanawajibishwa. Kwa upande wake, Mohamed Amin amesema DCI itafanya uchunguzi wa kina ili kuwakamata washukiwa, kuwafikisha mahakamani na kurejesha mali ya umma iliyopatikana kwa njia isiyo halali. Gatete Njoroge ana taarifa hiyo.