- 44,149 viewsDuration: 2:39Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wameanzisha uchunguzi kuwabaini na kuwasaka washukiwa wa ujambazi waliovamia saluni moja katika mtaa wa Saika, Nairobi, na kuiba zaidi ya shilingi elfu hamsini pamoja na simu ya mkononi. Washukiwa hao, ambao walinaswa na kamera za CCTV wakitekeleza uhalifu huo, walikuwa wamejihami kwa bunduki. Waathiriwa wameelezea hofu kuhusu usalama wao huku polisi wakisema wanaendelea na msako wa kuwakamata majambazi hao wawili. Franklin Wallah ana taarifa hiyo.