- 2,188 viewsDuration: 2:04Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imekanusha madai ya kinara wa DCP Rigathi Gachagua kwamba kampuni ya Korea Kusini ya Miru Systems imepewa kandarasi ya kusambaza teknolojia ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao katika njama ya wizi wa kura. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amewatahadharisha wanaotafuta zabuni hiyo kujiepusha na wanasiasa wanaotaka kuvuruga shughuli ya uchaguzi mkuu ujao.