- 3,519 viewsDuration: 2:48Familia moja mtaani Kawangware jijini Nairobi inalilia haki baada ya jamaa yao kupigwa na kuuawa katika eneo la burudani. Inaelezwa kuwa marehemu alivamiwa na wahudumu wa klabu hiyo kutokana na deni la shilingi elfu moja. Washukiwa watatu tayari wamefikishwa mahakamani na wanazuiliwa na polisi huku uchunguzi kuhusu tukio hilo ukiendelea. Franklin Wallah ana taarifa kamili.