- 2,667 viewsDuration: 3:20Familia moja katika eneo la Narumoru, Kaunti ya Nyeri, imegubikwa na majonzi kufuatia kifo cha mwana wao wa miaka miwili aliyefariki akiwa shuleni. Kulingana na familia hiyo, usimamizi wa shule unadai kuwa mtoto huyo alikanyagwa na gurudumu la nyuma la basi la shule baada ya kushuka kwenye gari hilo. Hata hivyo, mwalimu mkuu wa shule amesema ajali hiyo ilitokea wakati dereva alipokuwa akirejesha basi nyuma. Na kama anavyoarifu Emily Chebet, familia ya marehemu inasema maelezo yaliyotolewa na shule yanakinzana na ripoti ya polisi kuhusu mazingira ya tukio hilo.