- 1,485 viewsDuration: 3:02Familia ya Travis Wanjohi, mtoto wa miaka mitano ambaye mwili wake ulipatikana kando ya Mto Ragati huko Karatina, Kaunti ya Nyeri, inataka uchunguzi wa kina kufanywa ili kubaini kilichosababisha kifo chake. Ombi hilo linajiri baada ya asasi za usalama kueleza familia kuwa kisa hicho kwa sasa kinachunguzwa kama cha kufa maji, licha ya mwili wa mtoto huyo kupatikana katika hali mbaya siku 37 tangu kupotea kwake. Watetezi wa haki za watoto eneo hilo wametaka visa kadhaa vya watoto kupotea kuchunguzwa kwa kina.