- 6,833 viewsDuration: 2:46Familia moja ya Lucky Summer jijini Nairobi inadai haki baada ya mtoto wao, Alex Owegi Ariango, kufariki kutokana na majeraha ya kudungwa kisu akiwa katika shule ya Ruthimitu, Dagoretti South. Ariango amefariki miezi mitano baadaye baada ya kuugua kutokana na majeraha hayo. Familia inataka mshukiwa, ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule hiyo wakati wa tukio, akamatwe na kushtakiwa kwa mauaji.