- 2,921 viewsDuration: 3:08Familia ya mwathiriwa wa maandamano ya kupinga ujenzi wa kituo cha karantini ya Ebola katika kaunti ya Laikipia ingali kutambua mwili wake ambao umesalia katika makafani ya Hospitali ya Rufaa ya Nanyuki. Haya yanajiri huku majeruhi wa risasi wakijitokeza kudai haki na kuwalaumu maafisa wa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi. Waandamanaji waliokamatwa na kufikishwa mahakamani wameachiliwa kwa dhamana.